The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Mkoa wa Kigoma kuwa kitovu cha uzalishaji wa sukari Kanda ya Magharibi; wawekezaji wa ndani na nje wakaribishwa .


Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. Geoffrey Mwambe anawakaribisha wawekeza  ndani na nje ya nchi wenye nia ya kuwekeza  kwenye kilimo cha miwa na kiwanda cha kutengeneza Sukari kutumia shamba  lenye hekta 20,000 Wilayani Kibondo. Aidha katika kuhakikisha kwamba kiwanda kinapata malighafi ya kutosha pia wananchi watatumia eneo linguine lenye hekta 5,000 kwa matarajio kwamba watauza kwenye kiwanda kitakachojengwa. Hivyo kwa ujumla wake eneo hilo lina ukubwa wa hekata 25,000 kwa kilimo cha miwa na kiwandfa cha sukari katika kata ya Kibuye, Kibondo.

 

Kwa upande mwingine, pia Mwambe amewakaribisha wawekezaji  wenye nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha michikichi na kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kula  kutumia shamba ya Lugufu lenye hekta 10,529 na Basanza lenye hekta 3,249 yaliyopo Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma. Mashamba hayo yote tayari Serikali kupitia uongozi wa Halmashauri na Wilaya husika umeshayatenga kwa ajili ya uwekezaji huo. “Mashamba haya mawili  yametengwa na  serikali kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha zao la michikichi ili  kuzalisha mafuta ya kula ya mawese na kuondokana na changamoto ya kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi,”  Kwa mujibu wa  takwimu za Wizara ya Kilimo na Chakula  zinaonyesha  Tanzania inaagiza tani laki nne (400,000) za mafuta ya mawese huku ikitumia zaidi ya shilingi bilioni 600 kila mwaka kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi ili kufidia pengo la uhaba wa bidhaa hiyo hapa nchini” alisema

 

 

Kwa upande wa Kasulu uongozi unaendeleza majadiliano na mwekezaji kutoka India ambaye tayari ameonesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha miwa na kujenga kiwanda cha kuzalisjha sukari kwenye eneo lenye hekta takribani hekta 35,000.

 

 Mpango  wa nchi kwa sasa ni kuepuka kuagiza mafuta ya kula na sukari nje ya nchi pamoja na kupunguza gharama kubwa ya kuagiza bidhaa hizo ikiwemo fedha  nyingi za kigeni.

 

Mwishoni mwa wiki ya kwanza ya Aprili 2020. Mwambe amefanya ziara ya kikazi Mkoani Kigoma na  kufanya majadiliano na  Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Generali Mstaafu Emmanuel Maganga,  Mkuu wa Wilaya ya Uvinza  Mhe. Mwanamvua Mrindoko ,Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibondo  Mugishagwe  Rutema juu ya masuala mbalimbali ya uwekezaji Mkoani hapo. Kwa ujumla Mwambe amefurahishwa na utayari wa viongozi hao licha ya kuwakaribisha lakini pia kuwasaidia wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika Mkoa wa Kigoma  hususan kwenye mashamba yaliyotengwa na Serikali.

 

 

 

 

 

Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)