The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kinatoa tahadhari kwa Umma kupuuza na kuepukana na utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaotumia jina na nembo ya Kituo .


Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), kinatoa tahadhari  kwa Umma kupuuza na kuepukana na utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaotumia jina na nembo ya Kituo  kutapeli watu, kwa kujifanya wanasimamia Uwekezaji nchini. TIC ni Taasisi pekee ya Serikali yenye mamlaka ya kusimamia Uwekezaji nchini ikisaidiwa na Taasisi zingine za Serikali.

 

Kituo kinapenda kuutaarifu Umma/ Mwekezaji /Mdau mwenye nia ya kuwekeza au mwenye tatizo lolote kuhusiana na masuala ya uwekezaji awasiliane na Kituo kupitia  simu namba 0737 879 087 au, atembelee Tovuti yetu kwa anuani ya www.tic.go.tz au  Barua pepe: info@tic.go.tz au  Facebook; Tanzania Investment Centre au Instagram: invest_in_tanzania au Twitter: Investing Tanzania au YouTube: Uwekezaji Tv.

 

Ieleweke wazi kuwa suala la Uwekezaji halisimamiwi na mtu binafsi.

 

Kumezuka kundi la WhatsApp linalojiita *TANZANIA INVESTMENTS* ambalo linajinasibu kusimamia Uwekezaji nchini,kundi hili linajitambulisha kuwa linapatikana eneo la Nyanguge, Mwanza Mjini. Kundi hili  pia linatumia majina na nembo ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Pamoja na kuvunja Sheria za Nchi,kundi hili pia linafanya utapeli.Kituo kinaendelea na taratibu za kisheria ili kuweza kuwawajibisha waanzilishi na wanachama wa kundi hilo.

 

Ili kuepuka Matapeli, Kituo kinawashauri wadau wetu wa Mikoani kutumia Ofisi zetu za Kanda ambazo zimeanzishwa mahsusi ili kusogeza huduma karibu kwa wadau/wateja waliopo Mikoani.  Ofisi hizo za Kanda kwa sasa zimefikia saba (7). Yafuatayo ni maelezo ya Kanda hizo na mahali zilipo:-

 

1.Kanda ya Kusini yenye Ofisi zake Mkoani Mtwara (Jengo la Mkuu wa Mkoa) inayohudumia Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

 

2. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yenye Ofisi zake  Mkoani Mbeya (Jengo la Benki ya NBC) inayohudumia Mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe .

 

3.Kanda ya Kaskazini yenye Ofisi zake Mkoani Kilimanjaro(Ofisi za Mkuu wa Mkoa) inayohudumia Mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Tanga, 

 

4.Kanda ya Mashariki yenye Ofisi zake Dar es Salaam (Jengo la TIC Makao Makuu) inayohudumia Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.

 

5.Kanda ya Magharibi yenye Ofisi zake Mkoani Kigoma (Jengo la Mkuu wa Mkoa) na inahudumia Mikoa ya Rukwa, Katavi, Kigoma na Tabora.

 

6.Kanda ya Ziwa yenye Ofisi zake Mkoani Mwanza (Barabara ya Kenyatta), inayohudumia Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga,Geita na Simiyu

 

7.Kanda ya Kati yenye Ofisi zake Dodoma (Jengo la Manispaa) inayohudumia Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida.

 

Hizi  ndizo Ofisi za Kanda rasmi za TIC na kinawaomba wnaanchi Mikoani wazitumie zimeanzishwa kwa ajili yao.

 

Kituo kinaendelea kushughulikia matapeli hawa.

Kitengo cha Habari na Uhusiano TIC

   
Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)