The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Kampuni ya TCC imetumia vivutio vya uwekezaji kwa tija; imeongeza nguvu kwenye mtaji wa kuongeza mitambo zaidi ya kuzalisha sigara .


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji  Agellah Kairuki ametembelea  Kampuni ya Sigara Tanzania TCC ikiwa ni sehemu ya ziara yake kwa kampuni za uwekezaji ili kujionea hali ya uendeshaji/uzalishaji pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili na kutoa majawabu. Kampuni hiyo inamiliki kiwanda cha uwekezaji  kinachotengeneza sigara, bidhaa ambayo ina soko nchini na nje ya nchi. TCC ni mojawapo ya makampuni makubwa nchini yanayolipa kodi ya Serikali na kwa mwaka 2018 imelipa kodi zaidi ya shilingi bilioni 236.

 

Kampuni ya TCC imesajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC mwaka 2018. Kufuatia usajili huo, kampuni imenufaika na vivutio vya uwekezaji vinavyotolewa kwa wawekezaji. Jambo ambalo Kituo kinajivunia ni kwamba kwa kiasi kikubwa misamaha ya kikodi iliyotolewa kwa kampuni (kama vivutio vya uwekezaji), imetumika vizuri kama ongezeo la kwenye mtaji ambao umewezesha kuagiza mashine nyingine kwa ajili ya kuongeza zaidi uzalishaji wa  kiwanda. Kufuatia ongezeko la uzalishaji ni wazi pia kwamba uwezo wa kampuni  wa kulipa kodi pia utaongezeka kwa faida ya Taifa.

 

Waziri Kairuki ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika uwekezaji hasa wenye tija na kuwataka wawekezaji hao kutambua kuwa wamebeba dhamana ya nchi na watanzania. Hivyo muda wote wanapaswa kuzingatia utengenezaji wa bidhaa bora zinazokidhi matakwa ya walaji ndani na nje ya nchi.

 

“TCC mmebeba dhamana kubwa ya watanzania na nchi kwa ujumla kwani wananchi wanamiliki asilimia 22.8 huku Serikali ikimiliki asilimia 2.2, na asilimia 75 ikimilikiwa na Serikali ya Japan kupitia Kampuni yake ya Tumbaku JTI” alisema Waziri Kairuki.

 

Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)