The United Republic of Tanzania

TANZANIA INVESTMENT CENTRE

Wabunge wa Kamati mbili za Bunge walioshiriki semina ya TIC kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji kuwa Mabalozi wa uwekezaji


Wabunge wa Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma pamoja na Kamati ya Katiba na Sheria wamejengewa uwezo wa uelewa mpana wa masuala ya uwekezaji zoezi lililoendeshwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) huko Dodoma. Mgeni rasmi katika semina hiyo alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki. Semina ya TIC kwa Waheshimiwa Wabunge imeendeshwa ili kuwajengea uelewa mpana wa masuala ya uwekezaji hususan majukumu mbalimbali ya TIC kisheria. Majukumu hayo ni pamoja na kuhamasisha uwekezaji (wazawa na wageni), huduma zinazotolewa kwa wawekezaji kupitia mfumo wa huduma za mahala pamoja (upatikanaji wa ardhi, idhini ya vibali, leseni na vyeti vya uwekezaji), kuishauri Serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya uwekezaji nchini.

 

Akitoa neno katika semina hiyo, Mhe. Kairuki aliwaeleza....

2019-11-13 14:39:05Mhe. Balozi na Waheshimiwa Mabalozi Wateule ‘Tanzania ni sehemu sahihi ya kuwekeza’


4 Novemba,2019: Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimetembelewa na anayekwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Mhe. Balozi Inj. Aisha Amour na Waheshimiwa Mabalozi Wateule tisa  ambao hivi karibuni waliteuliwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwakilisha nchi nje ya nchi. Waheshimiwa hao wamefika na kupokelewa  na timu ya TIC ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mafutah Bunini kwa lengo la kuongezewa uelewa wa masuala ya uwekezaji wanapokuwa wakielekea kutekeleza na kusimamia masuala ya Diplomasia (Uwekezaji, Biashara na Utalii) nje ya nchi. 

 

Kipekee kabisa  Bw. John Mnali, Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji amewaeleza Waheshimiwa hao  taarifa za fursa za uwekezaji zinazonadiwa kwa sasa, mbinu za kuvutia uwekezaji, changamoto za uwekezaji  na miongozo stahiki ya namna ya kushawishi na kuvutia wawekezaji nchini katika hatua za awali. Sambamba na hayo pia....

2019-11-04 16:10:46Viongozi wamesikiliza, wamejibu, wameshauri na wameelimisha wafanyabiashra na wawekezaji Mikoa ya Kusini


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Angellah Kairuki ameongoza ziara ya pamoja ya viongozi katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara kati ya tarehe 23-27 Septemba, 2019. Ziara hiyo iliandaliwa pamoja na mikutano ya siku moja kati ya wawekezaji wafanyabiashara na viongozi. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kushiriki mikutano ya mashauriano kati ya Serikali na wafanyabiashara na wawekezaji katika ngazi za Mikoa ili kuibua kero/changamoto na kupatiwa majibu kutoka kwa viongozi husika wa Wizara, Taasisi na Mamlaka wanazosimamia. Kero na changamoto za biashara na uwekezaji katika maeneo ya ardhi, kodi, mazingira, nishati, maji, ardhi viliwasilishwa na kupatiwa majibu. Vilevile viongozi walitumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusiana na Ofisi zao na jitihada zinazochukuliwa na Serikali katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Aidha elimu juu ya umuhimu....

2019-10-07 10:07:12Misri yafikiria kuwekeza kwenye mradi wa magari nchini hatua itakayosaidia kupunguza uingizaji wa magari (used cars) kutoka nje ya nchi.


Ugeni wa takribani wafanyabiashara sita (6) kutoka Misri umefika nchini kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kuanzisha uwekezaji wao hapa nchini. Ugeni huo ni kutoka kampuni ya Ghabbour Auto na umeongozwa na Dkt. Raof Ghabbour ambaye ni  Mkurugenzi  Mkuu na Mwenyekiti wa kampuni hiyo. Ukiwa nchini kwa niaba ya Waziri Mkuu, ugeni huo umepokelewa na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki Waziri Mkuu, Dar es Salaam leo tarehe 18 Septemba,2019. Kikao pia kimehudhuriwa na Maafisa kutoka TIC na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Kampuni ya Ghabbour Auto huko Misri inajishugulisha na uzalishaji wa magari, uunganishaji wa magari sambamba na uzalishaji wa spea za magari. Katika mazungumzo na Mhe. Kairuki,  Mwenyekiti Dkt. Raof amesema kampuni hiyo ina nia....

2019-09-18 15:34:07Misri yafikiria kuwekeza kwenye mradi wa magari nchini hatua itakayosaidia kupunguza ungizaji wa magari (used cars) kutoka nje ya nchi.


Ugeni wa takribani wafanyabiashara sita (6) kutoka Misri umefika nchini kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kuanzisha uwekezaji wao hapa nchini. Ugeni huo ni kutoka kampuni ya Ghabbour Auto na umeongozwa na Dkt. Raof Ghabbour ambaye ni  Mkurugenzi  Mkuu na Mwenyekiti wa kampuni hiyo. Ukiwa nchini kwa niaba ya Waziri Mkuu, ugeni huo umepokelewa na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki Waziri Mkuu, Dar es Salaam leo tarehe 18 Septemba,2019. Kikao pia kimehudhuriwa na Maafisa kutoka TIC na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 

Kampuni ya Ghabbour Auto huko Misri inajishugulisha na uzalishaji wa magari, uunganishaji wa magari sambamba na uzalishaji wa spea za magari. Katika mazungumzo na Mhe. Kairuki,  Mwenyekiti Dkt. Raof amesema kampuni hiyo ina....

2019-09-18 15:26:58
Social Medias

Copyright ©2018 Tanzania Investment Centre.
All Rights Reserved.
Designed, Developed, and Maintained by Tanzania Investment Centre(TIC)