20 May, 2022
MINISTRY OF INVESTMENT, INDUSTRY AND TRADE, DEPUTY PERMANENT SECRETARY MR. S. ALLY GUGU MET WITH SWISS INVESTORS

Naibu Katibu Mkuu- Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Ally S. Gugu ameshiriki kikao na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Didier Chassot alipotembelea Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) akiwa ameambatana na Bw. Stefan Barny Mkurugenzi wa Taasisi ya Global Network pamoja na Bw. Daniel Schneider Mkuu wa Swiss Business Hub yenye Makao yake Makuu Nchini Afrika ya Kusini. Wawekezaji hawa wametoka nchini Uswisi.
Lengo la kikao hicho ni kujifunza fursa mbalimbali ambazo zinapatikana hapa nchini kwenye sekta za kiuzalishaji za utoaji wa huduma ili waweze kwenda kuhamasisha wafanyabiashara na wawekezaji ambao wapo Uswisi kuja kuwekeza hapa nchini.
Katika mkutano huu wa awali wameonesha kuvutiwa na Uwekezaji katika masuala ya uendelezaji wa nishati, masuala ya utaliii na usafirishaji hapa nchini.